Wednesday, July 23, 2014

0
POLISI YAMSHIKILIA MWANDISHI WA HABARI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA


Kijana aliyetambulika kwa jina la Musa Mbeko(24) anayedaiwa kuwa ni mwandishi wa habari mkoani Tabora akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kujifanya kuwa ni afisa kutoka idara ya usalama wa taifa (TISS).kijana huyo inadaiwa aliwahi kufanya kazi kituo cha radio cha Voice of Tabora (VOT) kinachomilikiwa na mbunge wa Jimbo la Tabora mjini,Ismail Rage,hata hivyo Uongozi wa VOT umekana kijana huyo kuwa ni mwandishi wao na kwamba ulikwisha mfukuza kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya Utapeli
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa.
 . 
Kitambulisho alichokuwa akitumia kijana Musa Mbeko.
Kijana Musa Mbeko akiwa mbele ya kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzana Kaganda.
Kijana Musa Mbeko akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Polisi.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
WAZIRI DKT BINILITH MAHENGE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MAGOGO KWA WAWEKEZAJI


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uzalishaji soda Bw. Louis Coetzee ( wa kwanza kulia), akielezea jinsi kiwanda hicho kinavyotumia maji taka kulinda Mazingira ya kiwanda.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dkt. Injinia Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake na kuwaambia kwamba nchi inahitaji wawekezaji wanaotunza na kulinda Mazingira yetu. Viwanda alivyovitembelea ni kiwanda cha kuzalisha Mafuta ya kula na sabuni (BIDCO), M.M.I steel mill kinachozalisha Nondo na Mabati pamoja na kiwanda cha Coca Cola vilivyopo Mikocheni  jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge, akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha Coca Cola (hawapo pichani)  kuhusu kiwanda hicho jinsi walivyoweza kutunza Mazingira na kuwataka waendelee kuboresha zaidi Mazingira ya kiwanda na kuwa mfano wa kuigwa kwa viwanda vingine.
 Maji machafu yenye kemikali  yanayotiririka kutoka kwenye kiwanda kinachozalisha Nondo na Mabati (M.M. I steel mill ) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam ambayo si salama kwa wananchi na mazingira kwa ujumla.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano  Mahenge ( wa pili kulia)  pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu (wa kwanza kushoto), wakiwa katika ziara  fupi ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha Coca Cola kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Wakiwa pamoja na mkurugenzi wa uzalishaji soda katika kiwanda hicho Bw. Louis Coetzee (wa kwanza kulia).

========== =======   ========

Wawekezaji wote Nchini wanatakiwa kuhakikisha wanaacha kutumia magogo katika uzalishaji badala yake watumie tekinolojia ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya tabia ya nchi  na uchafuzi wa Mazingira yanayotokana na ukataji miti. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Mh.Dkt. Injinia Binilith Mahenge wakati  alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia (BIDCO) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.

Amekiagiza kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya magogo kwani inaathari kubwa sana kwa jamii.  Hata hivyo amesema kuwa atatembelea tena kuangalia kama wameacha kutumia magogo ndani ya miezi sita, endapo watabainika wanaendelea kutumia magogo,hatua kali itachukuliwa juu ya Kiwanda hicho endapo watakiuka masharti waliyopewa  Kiwanda kitafungwa mara moja.

Hata hivyo Mh. Mahenge amewaomba wawekezaji wa viwanda vingine kuiga mfano wa kiwanda cha Coca Cola katika utunzaji wa Mazingira, kwani wao ni mfano mzuri kwa viwanda vingine kwa kuanzisha technolojia nyengine ya kuchunguza maji taka kama ni salama kwa viumbe hai.

Amemalizia kwa kusema "Tunapenda wawekezaji lakini ni wale wanaotunza na kuyaenzi mazingira kwa usalama wa wananchi na nchi yetu kwa ujumla".
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
=========  =========  =========
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
23/7/2014. Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya  Mashujaa  itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yamekamilika na kuongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu kihistoria  yanalenga kuwaenzi wote waliojitoa muhanga katika jitihada za  kuikomboa ardhi ya Tanzania, kuilinda na kudumisha amani na utulivu uliopo.

Amesema  maadhimisho  hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Gwaride la Kumbukumbu litakaloonyeshwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na uwekaji na silaha za asili, maua kwenye mnara wa kumbukumbu pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoa dua na sala kuliombea taifa.

Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja huo.

Aidha, katika hatua nyingine ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo  barabara ya Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
MKUU WA SHULE ILIYOONGOZA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA 6 AHAMA NYUMBA ILI WANAFUNZI WAPATE PA KULALA

SHULE ya Igowole, iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu, inakabiliwa na matatizo mengi, ikiwemo ukosefu wa mabweni, kiasi cha Mkuu wa Shule kulazimika kuhama nyuma kuachia wanafunzi wapate pa kulala.

Mbali na ukosefu wa mabweni ya kuhimili idadi ya wanafunzi, matatizo mengine ya shule hiyo ni ukosefu wa maji, maktaba, vifaa vya kufundishia na kusomea, gari la shule na walimu hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mkuu wa shule hiyo ya serikali iliyoko katika Kijiji cha Igowole wilayani Mufindi, Andrew Kauta, ameachia nyumba kwa ajili ya sehemu ya wanafunzi wa kike 237 wanaojiunga na kidato cha tano shuleni hapo.

Hata hivyo, shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988 na kidato cha tano na sita kuanza mwaka 2008, pamoja na matatizo hayo, imeongoza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu, yaliyotangazwa hivi karibuni.

Kati ya wanafunzi 30 waliohitimu Kidato cha Sita mwaka jana, 19 walipata daraja la kwanza, 10 daraja la pili na mmoja ndiye mwenye daraja la tatu.

Kitendo cha kuibuka na matokeo mazuri, licha ya kuwepo changamoto hizo, kimekuna wadau wengi akiwemo Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola ambaye amesema mafanikio ya shule hiyo yanaonesha jinsi walimu na wanafunzi wake wasivyokatishwa tamaa.

Alisisitiza upo umuhimu mkubwa wa kupewa misaada wanayohitaji ili wafanye vizuri zaidi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkuu wa Shule alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, haijawahi kupokea wanafunzi wengi wa Kidato cha Tano kama ilivyotokea mwaka huu.

“Tangu elimu ya kidato cha tano na sita ianze kutolewa shuleni hapa mwaka 2008, tumekuwa tukipokea wastani wa wanafunzi 30 wa kidato cha tano kila mwaka,” alisema Mkuu huyo.

Alisema mwaka huu, shule hiyo imeletewa wanafunzi wa kike 237 wa Kidato cha Tano, watakaoungana na 30 walioingia kidato cha sita. Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 900 kidato cha kwanza hadi cha sita.

Hata hivyo, mkuu huyo alisema shule ina bweni moja pekee lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiozidi 86. Alisema bweni hilo lililojengwa tangu shule ilipoanzishwa, miaka 26 iliyopita, haliko katika hali nzuri.

Alisema wanafunzi takribani 30 wa Kidato cha Tano, watajibana katika nyumba hiyo huku wengine 36 wakipelekwa katika bweni hilo pekee. Wanaobaki watahifadhiwa katika madarasa matatu, yanayotumiwa na wanafunzi wa vidato vya chini.

Mwalimu wa Taaluma, Isiaka Chodota alisema kutokana na sehemu ya madarasa kutumika kama mabweni, shule inabakiwa na vyumba 19 vya madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu na Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola waliahidi kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya shule hiyo, waliyoieleza kwamba mafanikio yake yameutoa kimasomaso mkoa wa Iringa.

Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule hiyo katika matokeo ya Kidato cha Sita, Mkuu wa Shule alisema mwaka 2010 walijiwekea mpango mahususi wa miaka mitano wa kuboresha elimu katika shule hiyo, ikiwa ni pamoja na kusisitiza matumizi ya Kiingereza.

Siri nyingine ya mafanikio ya shule hiyo ni kuipa kipaumbele nidhamu. Kwa mujibu wa mkuu wa shule, kila Ijumaa huhakikisha wanafunzi na walimu wanakumbushwa sheria, kanuni na miiko ya shule.

Chanzo: Habarileo
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
MWANAMKE KICHAA AKUTWA NA MAITI YA MTOTO WA MIAKA MITANO NA HIRIZI KIBAO

Katika hali ya kushangaza mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili (pichani ) amekutwa na maiti ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano katika mji wa Lagos nchini Nigeria mapema leo asubuhi.
 
Mbali na kukutwa na maiti ya mtoto huyo,kichaa huyo pia amekutwa na rundo la hirizi
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
MABWENI YA SHULE YATEKETEA KWA MOTO MONDULI ARUSHAWANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo asubuhi.
 
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ulizuka wakati wanafunzi hao wakiwa darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
 
Kikosi cha Zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea. Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha mabweni hayo katika hali ya kawaida.
 
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
WAKUU WA SHULE ZILIZOFANYA VIBAYA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2014, WAPEWA MWEZI MMOJA KUJIELEZA
Wakuu wa shule za serikali zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu  pamoja na Maofisa elimu wa Mikoa wamepewa muda wa mwezi mmoja ili kubaini chanzo cha  shule zao kuwa na ufaulu hafifu.
 
Baada ya kubaini chanzo hicho cha ufaulu hafifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI.
 
Miongoni mwa shule ambazo wakuu wake wametakiwa kujieleza ni pamoja na shule ya Tambaza iliyopo jijini Dar es salaam na shule ya Iyunga ya Mkoani Mbeya, ambapo muda huo wa mwezi mmoja umeanza  leo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,  katibu Mkuu Tamisemi Jumanne Sagini amesema, kushuka kwa ufaulu kwa shule hizo kumewashtua  watu wengi, kwani shule hizo zimejengewa uwezo mzuri wa vifaa pamoja na miundombinu.
 
Hata hivyo Sagini amesema, idadi ya wanafunzi 22,685 waliofaulu masomo ya sayansi kwa mwaka  huu wa 2014  ni kubwa kwa  zaidi ya wanafunzi 3,939 ikilinganishwa na wanafunzi 18,746  waliofaulu masomo hayo mwaka jana.
 
Amesema kuwa ufaulu huo umeipa changamoto Serikali na imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ambae amefaulu na kupata alama stahiki  katika masomo aliyoyachagua anapata shule.
 
Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamepangiwa kusoma masomo ya sanaa ilihali ufaulu wao ni katika masomo ya sayansi, kutokuwa na wasiwasi kwani serikali imebaini changamoto hiyo na kuifanyia kazi.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
"MAFANIKIO YETU YANATOKANA NA WANAUME AU WAPENZI WETU" ASEMA AUNT EZEKIELSTAA wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, amesema mafanikio ya wasanii wengi wa kike hayatokani na mauzo ya kazi hiyo bali sapoti ya waume au wapenzi wao kwa kuwa soko la filamu limeharibika.
 
“Filamu kwa Tanzania hakuna soko, walau wanaume, si wanawake, huwezi kunilinganisha mimi na Ray… Mimi kama si kuwa mwanamke, sidhani kama leo hii bado ningekuwepo katika filamu, kwa sababu kwa kiasi kikubwa nategemea sapoti ya wadau wangu, si mauzo ya filamu,” alisema.
 
Aunt alisema tatizo jingine katika soko la filamu nchini, ni wasanii kutopendana hali ambayo inashusha tasnia kila kukicha. Kwamba wangekuwa na mshikamano, wangeweza kufanya kitu cha kuwasaidia katika kuiboresha.
 
“Umoja ndiyo kila kitu hata kama tutakuwa hatuna hela, lakini tukikaa watu wengi kujadili kitu fulani, tutajua tufanye nini, hata kimawazo tu tutaendelea,” alisema.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
NYUMBA 4 ZACHOMWA MOTO KWA TUHUMA ZA USHIRIKINAWakazi wa kijiji cha Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wamechoma nyumba nne za familia moja yenye zaidi ya watu ishirini na kuteketeza vyakula na mali nyingine zenye zaidi ya shilingi milioni mia moja baada ya kumtuhumu mmoja wa wanafamilia kwa ushirikina.
 
Mwenyekiti wa kitongoji cha mkoronga katika kijiji cha nguruka Matei Charles ambaye alimuokoa mtuhumiwa wa uchawi aliyetambulika kwa jina la Siyajui Ahmad , amesema mama huyo alianza kushambuliwa akiwa katika msiba wa kijana Masoud Vyombo ambaye alifariki ghafla ambapo wakazi wa kijiji hicho waliomtuhumu kumuua kwa njia ya ushirikina walianza kumshambulia kabla ya kuokolewa.
 
Mamia ya wananchi waliamua kuteketeza nyumba yake pamoja na nyumba tatu za kaka zake na wazazi wake, huku mtuhumiwa akieleza kuwa familia hiyo imepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia moja na kwamba alilazimika kutoroka ili kuokoa maisha yake.
 
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Frasser Kashai amesema jumla ya watu kumi na watano wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku kwa upande wake katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Uvinza Majaliwa Zuberi akitoa wito kwa wananchi kutochukua sheria mkononi na akaitaka kamati ya maafa ya wilaya kuzisaidia familia Nne zilizoathirika ambazo kwa sasa zinalala nje na hazina chakula, mavazi na mahitaji mengine ya msingi.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
KIFO CHA MKE WA ASKARI POLISI ALIYEFIA KWA DEREVA BODABODA BADO NI UTATA


Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga.

Wingu zito limegubika kifo cha mke wa askari polisi wa wilayani Mwanga, Kilimanjaro aliyefia chumbani kwa dereva wa bodaboda.

Uchunguzi wa awali wa polisi unadai kuwa mwanamke huyo alilala chumbani huko usiku mzima wa kuamkia Jumapili, siku ambayo maiti yake iligunduliwa saa 12 jioni. 
 
Uchunguzi huo pia unadai kuwa mtuhumiwa ndiye aliyempigia simu shangazi ya mwanamke huyo na kumuita nyumbani kwake kwa dharura.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema jana kuwa baada ya shangazi kufika, alishuku jambo baada ya kuona mtuhumiwa anaweweseka bila kumweleza alichomwitia.
 
“Akiwa amesimama nje ya chumba cha huyo bodaboda ambaye alionekana kama mlevi hivi, aliona kwa ndani kukiwa na mwanamke aliyekuwa amelala sakafuni,” alisema na kuongeza kuwa shangazi huyo aliamua kusukuma mlango ndipo alipomkuta mtoto wa kaka yake akiwa amelala sakafuni.
 
“Shangazi aliita majirani na katika hekaheka hiyo polisi waliitwa na kukuta mwanamke huyo akiwa amekufa na ndani ya chumba kulikuwa kumezagaa paketi za pombe,” alisema.
 
Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi wilayani Mwanga huku taarifa ya chanzo cha kifo hicho zikisubiri uchunguzi wa mwili wa marehemu.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

Tuesday, July 22, 2014

0
TAARIFA RASMI YA MTOTO ALIYENYONGWA NA KUTUPWA KISIMANI WILAYANI KAHAMA

Mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na wiki tatu amekutwa amefariki dunia baada ya kunyongwa na kutupwa na mama yake katika kisima kilichopo mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea jana asubuhi mjini kahama.

Kamanda Kamugisha amesema mama wa mtoto huyo Rhoda Idedemya (18) mkazi wa Nyasubi ametenda tukio hilo na kujaribu kutoroka kabla ya kukamatwa na jeshi la polisi akiwa ndani ya gari la abiria liendalo Runzewe.
Mama wa mtoto huyo Rhoda Idedemya akiwa katika kituo cha polisi Kahama baada ya kukamatwa.
Mama mlezi wa mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina la Christina au mama paulo amesema ameishi na mtuhumiwa huyo toka akiwa na ujauzito baada ya kumuomba hifadhi mpaka alipojifungua wiki tatu zilizopita.

Amesema Rhoda amekuwa na tabia ya kuondoka nyumbani na kumuacha mtoto zaidi ya masaa matano,na baada ya kukemewa alikiri kutorudia.

Christina amesema, hii leo akiwa kazini kwake,Rhoda alimfuata na kumuaga kuwa anakwenda Runzewe kwa kaka yake, na kwamba mtoto amempeleka kwa baba yake anayeishi mhungula hali iliyompa wasiwasi na kufuatilia hadi alipokutwa ndani ya gari la abiria liendalo runzewe.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya kahama, na mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi uchunguzi utakapo kamilika. 
 Kisima alichotupwa mtoto huyo
Majirani wakiwa katika nyumba aliyokuwa anaishi mama wa mtoto huyo
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
AMINA MAIGE ANAYESHTAKIWA KWA KUMG'ATA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI LEO

Kesi inayomkabili Amina Maige kwa kosa la kumng'ata na kumchoma kwa pasi mfanyakazi wake wa ndani Yusta Lucus miaka ishiriani haikuweza kusikilizwa na mahakama ya kinondoni baada ya mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.

Kesi hiyo inayomkabili Bi Amina Maige imeshindwa kuoendelea kama ilivyopangwa licha ya mashahidi wawili pamoja na mwathirika wa tukio hilo kufika mahakamani hapo kwa madai kuwa mshtakiwa mgonjwa ambapo wadhamini wa mtuhumiwa walihudhuria makahamani hapo.
 
Hakimu mkazi Flora Mtarania ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 13 Agusti mwaka huu.
 
Wakati huo huo kesi ya wizi wa mamilioni ya shilingi katika benki ya Barclays inayowakabili washtakiwa 12 wakiwemo washtakiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Mtawa wa kanisa katoliki imetajwa katika mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam.
 
Washatakiwa hao wamepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu Nyigulila Mwaseba wakituhumiwa kwa kesi ya unyang`anyi wa kutumia silaha na wizi wa shilingi milioni mia tatu tisini nukta mbili,dola 55 elfu za kimarekani na yuro elfu mbili mia moja na hamsini katika bank ya Barclays tawi la kinondoni ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi August 05,mwaka huu.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
WANANCHI WAWATIMUA VIONGOZI WA CCM KWENYE MKUTANO WILAYANI RUNGWE

WANANCHI wa Kata ya Kambasegela wilayani Rungwe mkoani hapa, wamewafukuza viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wa kata hiyo walipotaka kufanya mkutano wa hadhara ili kuimarisha chama chao.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga, Katibu wa jumuiya hiyo Kata ya Kambasegela, Frank Mwansasu, alisema wananchi walimtimua yeye na msafara wake kwa madai kwamba waliahidiwa maji zaidi ya miaka kumi sasa bila kupatiwa.

“Mwenyekiti, kero yangu kubwa ni kwamba, mimi na wenzangu tulifukuzwa na wananchi tusifanye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yetu ya kata, wananchi wanasema waliahidiwa maji, lakini hawajapelekewa mpaka hivi sasa,” alisema Mwansasu.

Akijibu kero hiyo, Mwenyekiti Kasenga, alisema hayo ni matokeo ya baadhi ya viongozi kutowajibika vema katika nafasi zao.

Alisema suala hilo limemsikitisha, na kwamba yeye na msafara wake watalifikisha kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi, ili kulipatia ufumbuzi.

Akiwa katika ziara hiyo, mwenyekiti huyo alipokea kero nyingine kwa baadhi ya wananchi wa Kata ya Nkunga, ambao walimwambia kuwa chama hicho kinachukiwa kwa udhaifu wa baadhi ya viongozi wake.

Wananchi walisema kata hiyo ina uhitaji wa umeme, na kwamba katika Kijiji cha Ibililo, kuna msigano wa viongozi, jambo ambalo linasababisha kutopatikana kwa maendeleo ya kijiji.

“Jitokezeni kwenye marekebisho ya daftari la kudumu la mpiga kura na ukifika wakati wa uchaguzi, wazee, vijana na wanawake wanaofaa wapeni nafasi wagombee,” alisema Kasenga.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
SERIKALI YAPEWA "BIG UP" KWA KUYANG'OA MABANGO YA WAGANGA WA KIENYEJI

CHAMA cha Utabibu wa Dawa Asili (ATME) Mkoa wa Dar es Salaam, kimepongeza hatua ya serikali kuanza kuyang’oa mabango ya waganga wa kienyeji na kuomba ushirikiano zaidi, ili kufanikisha zoezi hilo  nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa ATME Mkoa wa Dar es Salaam, Rafael Nyampiga, alisema zoezi hilo litakapomalizika jijini Dar es Salaam, waratibu wa ATME, viongozi wa serikali kutoka manispaa zote  watakutana, ili kujadili changamoto na hatua zaidi za kufanya kufanikisha jambo hilo.

Nyampiga alisema zoezi hilo limeanzia kwa sasa limeanzia Wilaya ya Temeke, kubaini waganga 30 wanaofanya kazi kinyume na sheria na kusema kuwa wanaamini kama watashirikishwa vilivyo watakamatwa wengi zaidi.

“Sisi ndio tunaishi na watu hawa na tunajua mbinu zao zote za ufanyaji kazi kwa utapeli, lakini kama mnavyojua sisi wenyewe au serikali yenyewe haiwezi kufanikiwa bila ushirikishwaji wa karibu wa pande zote mbili,”alisema.

Katika hatua nyingine, alikiri baadhi ya namba zinazowekwa kwenye mabango huwa hazipatikani, lakini kwa kutumia wateja wao waganga wanaofanya kazi kwa utapeli ni rahisi kukamatwa.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>

0
WATU 8 WATIWA MBARONI KUHUSIANA NA SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYONASWA DARKamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na Vyombo vya habari mbalimbali mapema leo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar kuhusiana na sakata la viungo vya binadamu vilivyokamatwa jana ambapo Kamanda Kova amesema kuwa watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

 Kamanda Kova amesema kuwa jopo la Wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo vile vilikuwa ni vya maiti,ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.
BONYEZA HAPA KWA HABARI KAMILI>>>